KL106 : Dunda mpira kuelekea kwenye goli (kikapu) + Zungusha mwili kwa ndani uelekeo wa goli + Zuia mpira kwa mkono mmoja kisha pitisha nyuma ya mwili na upokee kwa mkono mwingine + Kugusa shingo + Malizia kwa layup kiganja kikiwa juu ya mpira
tafsiri: Bahati Mgunda
Bball-shorthand
Dunda mpira kwanza kwa
kuuzungusha ili ukurudie baada ya kudunda
Ruka na daka mpira, tua chini kwa miguu yote kwa pamoja
“kama Bata anavyotua” miguu iwe umbali sawa na upana wa kifua chako na miguu ikielekea upande lilipo goli
Piga hatua mbele kwa mguu mmoja kuelekea upande ulipo mguu mwingine
Dunda mpira kwakutumia mkono ulipo upande ambao unaelekea. Mpira udundwe kwa wakati mmoja na hatua inapopigwa, hii itasaidia kuulinda mpira.
Zungusha mwili kwa ndani uelekeo wa goli
mwili uzunguke nyuzi 270 kwa ndani
Zuia mpira kwa mkono mmoja kisha pitisha nyuma ya mwili na upokee kwa mkono mwingine
hakikisha mkono umenyooka kabisa wakati wa kuzungusha na kupokea mpira.
Piga hatua kuelekea kwenye goli
ukijitayarisha kwa ‘layup’ baada ya hatua mbili
Kugusa shingo
Gusa shingo kwa nyuma na mpira ulioshikwa kwa mikono yote miwili kupitia juu ya kichwa na kuurudisha tena mbele
Malizia kwa layup kiganja kikiwa juu ya mpira
malizia kwa mpira kugonga bodi ukilenga kwenye kona ya juu ya mraba.
sauti: Google Translator